KUWASA PAMOJA NA KAMPUNI AFRICAN ONE CONSTRUCION WASAINI MKATABA WA MRADI MAJI KAHAMA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Sunday, 5 May 2024

KUWASA PAMOJA NA KAMPUNI AFRICAN ONE CONSTRUCION WASAINI MKATABA WA MRADI MAJI KAHAMA

Mkuu wa Wilaya Kahama Mkoa Shinyanga Mboni Mhita amewataka wananchi wa mtaa wa Mtakuja Kata ya Nyahanga kuwa waaminifu na kulinda miundo mbinu ya maji ili kutoisababishia serikali hasara.


Mboni ameyasema hayo wakati wa utiaji saini wa mkataba wa mradi wa maji Mtakuja uliofanywa kati ya Mamlaka ya Maji safi na usafi wa mazingira Kahama (KUWASA) na Kampuni ya Afrika one construction.


Naye Frank Moses Mtangi kutoka Kampuni ya Afrika one construction ameshukuru kupata mradi huu na atatekeleza kama ulivyopangwa pia amesema vijana watapata ajira ndogo ndogo wakati mradi huo ukitekelezeka.


Baadhi ya wananchi wa mtaa wa Mtakuja Magdalena Charles na Denisa Kulige wamesema mradi huo ukikamilika utawasaidia kuondoa adha waliyonayo kwa sasa ambapo wanatumia umbali mrefu kufuata maji na wakati mwingine wananunua maji kwa wauzaji ambapo pipa moja lina gharimu shilingi elfu tatu.


Mradi huo utagharimu kiasi cha shilingi milioni 184 mpaka kukamilika na unatarajiwa kuhudumia Kaya 2500 zilizopo Mtaa wa Mtakuja Kata ya Nyahanga Manispaa ya Kahama.





No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso