Haruna Iddi katibu wa nzengo ya Mtaa wa Malunga akizungumza na waandishi wa habari
NA NEEMA NKUMBI- HUHESO DIGITAL KAHAMA
Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga linamshilikia Jafari Magesa Miaka 31 Mkazi wa Milambo kwa tuhuma za kuunda njama za kumuua mtalaka wake na kitu chenye ncha kali aitwaye Gaudensia Shukuru miaka 25 Mkazi wa Malunga Manispaa ya Kahama.
Adelina Shukuru Dada wa marehemu akizungumza na waandishi wa habari
Kamanda wa Polisi Mkoani Shinyanga Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi hilo Janeth Magomi amesema tukio hilo limetokea May 27 mwaka huu baada ya kupokea taarifa toka kwa Mwenyekiti wa kitongoji cha Wendele ya uwepo wa Mwili wa Mwanamke aliyeuwawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali
SACP Magomi amesema kuwa katika upelelezi wa awali wa chanzo cha tukio hilo ni mgogoro wa Talaka kati ya marehemu na aliyekuwa mumewe ambapo walikuwa na kesi Mahakamani juu ya Talaka ambayo ilikuwa itolewe hukumu yake May 28, 2024.
Kwa upande wake Haruna Iddi katibu wa nzengo ya Mtaa wa Malunga ambapo marehemu Gaudensia alipokuwa anaishi amesema kuwa msiba huu haupo katika taratibu ambazo tumezizoea za mwenyezi Mungu kwa maana aliyefariki amekatiliwa uhai wake kwa kuchinjwa na kutobolewa macho hivyo sio mapenzi ya Mungu
Ameongeza kuwa visa hivi si kwa Mtaa huo tu bali ni Tanzania nzima kwa ujumla yanatokea Watu wanajichukulia sheria mkononi na kutoa uhai wa wenzao kitu ambacho si sawa kwa mujibu wa sheria zetu za nchi hata vitabu vya dini hivyo ameiomba serikali kuwachukulia hatua kali wanaofanya mambo ya kikatili ili kupunguza hatari hii kwa wananchi
Naye Adelina Shukuru Dada wa marehemu ameeleza jinsi alivyoweza kuupata mwili wa Dada yake ambapo amesema kuwa alikuwa hajamwona toka jumapili na alijaribu kumtafuta bila mafanikio ndipo alipoenda kutoa taarifa siku ya jumatano hatimaye kupata mwili huo ukiwa umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya manspaa ya Kahama
No comments:
Post a Comment