Kwa muda mrefu wananchi wa Kata za Ruhembe, Kidodi, Uwembe, Vidunda, Mikumi na Kilolo, Mkoani Morogoro wameteseka kwa kusafiri umbali mrefu au kuzunguka kwenye mapori ya miwa kufikia huduma za kijamii.
Hali hiyo ilitokana na kukosekana kwa kiunganishi
madhubuti ya miundombu ya barabara katika
kata hizo.
Akizungumza
wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengewa, Mbunge wa Jimbo la Mikumi Mhe. Denis
Londo amesema wananchi hao walitumia gharama kubwa katika kuzalisha mazao yao.
"Hadi mkulima anakuja kuuza mazao yale hapati
faida kwa kuwa ametumia gharama kubwa wakati wa kupanda na kukuza mazao yake
kutokana na kukosekana kwa miundombinu rafiki." amesema Mhe. Londo
Mhe. Londo ameishukuru Serikali kwa ujenzi wa
Daraja la Luhembe ambalo kwa kiasi kikubwa litampunguzia mkulima gharama za
uzalishaji.
Akizungumza katika ziara hiyo Meneja wa TARURA
Mkoa wa Morogoro Eng. Emmanuel Ndyamkama amesema daraja hilo litakua na urefu
wa mita 40 na litagharimu takribani Sh bilioni 1.2.
Akitoa maelekezo wakati wa ziara hiyo, Mhe
Mchengerwa amewataka TARURA Mkoa wa Morogoro kuhakikisha ujenzi wa daraja hilo
unakamilika kwa wakati na kuwataka kujenga barabara za lami zenye urefu wa mita
100 kwa kila upande kuunganisha daraja hilo.
"Nimeona ujenzi unaendelea vizuri sasa na
mmeniambia kuwa mmepanga kujenga barabara za kuunganisha daraja hilo zenye
urefu wa mita 15 sasa niwatake muongeze zifikie mita 100 kila upande."
amesema Mhe. Mchengerwa
"Pia ongezeni kuweka na taa za barabara kumi
kwa pande za kuingilia na kutokea kwenye daraja ili kuwe na mwanga wakati wote."
amesema Mhe. Mchengerwa
Mhe. Mchengerwa amesema
katika kuzuia mmomonyoko katika eneo linalojengwa daraja ameitaka TARURA kuweka
‘Gabions’ za kutosha.
Mhe. Mchengerwa yuko katika ziara ya kazi mkoani Morogoro na
ameshatembelea Halmashauri za Wilaya ya Kilosa na Ifakara Mji.
No comments:
Post a Comment