BASHE KUONGOZA MKUTANO WA WADAU WA TASNIA YA MBEGU LEO DODOMA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday 24 May 2024

BASHE KUONGOZA MKUTANO WA WADAU WA TASNIA YA MBEGU LEO DODOMA








Na Nyabaganga Taraba - Dodoma

Mkutano Mkuu wa wadau wa Tasnia ya mbegu Tanzania unafanyikaleo Jijini Dodoma ambapo mgeni rasmi ni Waziri wa Kilimo Mhe Hussein Bashe.

Miongoni mwa mada zitakazowasilishwa kwenye mkutano huo wadau wa Tasnia ya mbegu ni Hali ya Tasnia ya mbegu na mpango wa uendelezaji mbegu, Majukumu ya SAGCOT katika kuwezrsha upatikanaji wa mbegu za mazao ya biashara na viazimviringo na Mikakati ya kuwezrsha upatikanaji wa mbegu za awali za mazao mbalimbali.



Mada zingine ni fursa za biashara ya mbegu Bora'' za mazao ya Kilimo , uthibiti wa ubora wa mbegu,fursa za ajira za wanawake na vijana kupitia Tasnia ya mbegu, upatikanaji wa mbegu Bora'' za mazao ya mbogamboga na Miche Bora'' ya miti ya matumda na mada ya kujengea uwezo wazalishaji mbegu kupitia BBT.

Baada ya Majadiliano wadau hao watatoka na maazimio ya pamoja lengo likiwa yale watakayokubaliana yatatekelezwa.

Aidha maonesho ya wadau wa mbegu yapo katika eneo la viwanja vya Hotel ya Morena Jijini Dodoma.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso