MENEJA Habari na Mawasiliano wa Yanga , Ally Kamwe amesema klabu hiyo inadhamiria kuanzisha utaratibu wa kuruhusu watoto chini ya umri wa miaka 10 kuingia uwanjani bure kwenye michezo ya timu hiyo.
Akizungumza na HabariLEO mapema leo, Ally Kamwe amesema lengo ni kutengeneza mashabiki na Wananchi imara kwenye timu hiyo kwa miaka ya baadaye.
“Na unajua mtoto unavyomrisisha mtafutie ‘moment’ (wakati) mzuri huwezi haiwezi kuja mechi kama ‘derby hii’ ukamwambia njoo, hapana unaangalia mechi fulani hawa watoto wanaowaskia Max Zengeli, Pacome Zouzoua waje wawaone,” amesema Kamwe.
Kamwe amesema kama klabu hiyo ikifanikiwa kuchukua ubingwa mapema watu wategemee kuona uhusiano wa karibu na wadau wa klabu hiyo.
No comments:
Post a Comment