Mbunge wa Jimbo la Sengerema, Hamis Tabasamu amelalamikia umakini mdogo wa upimaji magari barabarani na kuitaka Wizara ya Ujenzi kuja na majibu sahihi.
Tabasamu amesema hayo leo Bungeni jijini Dodoma wakati akichangia Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
"Hizi mizani zilizopo barabarani zinazuia kabisa uwekezaji. Gari la mafuta linabeba lita elfu arobaini na mbili na hakuna chochote ambacho kimezidishwa pale halafu unaambiwa gari limezidi (uzito)! Nilisafiri kwenye basi lina 'level seat' (hakuna aliyesimama). Basi lile lilipimwa mizani ya Usagara, linakuja kupimwa tena katika mizani nyingine ya Tinde limeonekana limezidi kilo 60.
Abiria tunazidiana, mwingine ana kilo 150 mwingine 120 (hivyo) wenye mabasi watawezaje kuwapima abiria?" amehoji Tabasamu.
No comments:
Post a Comment