WAZIRI MKUU AWAPONGEZA KILIMANJARO KWA KUTOKUWA NA UDUMAVU WA WATOTO - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday, 2 April 2024

WAZIRI MKUU AWAPONGEZA KILIMANJARO KWA KUTOKUWA NA UDUMAVU WA WATOTO


Waziri Mkuu, Kasimu Majaliwa ameupongeza Mkoa wa Kilimanjaro kwa kutokuwa na udumavu wa watoto utokanao na lishe huku akisisitiza kuendelea na ulishaji bora.

Majaliwa amesema kwa mujibu wa takwimu ya mwaka 2022 hali ya lishe Tanzania si ya kuridhisha kwa kuwa inaonyesha asilimia 30 ya watoto walio chini ya miaka mitano wanakabiliwa na tatizo la udumavu, asilimia 12 wana na uzito pungufu na asilimia tatu wana ukondefu.

“Tumeendelea kusisitiza chakula kiwe na virutubisho vyote, wanawake walio kwenye umri wa kuzaa, wajawazito wanaonyonyesha, wasichana balehe na watoto wenye umri chini ya miaka mitano ni muhimu wakapata lishe bora,”amesema Majaliwa.

Ametaja mikoa 12 inayoongoza kwa udumavu wa watoto chini ya miaka mitano ambao wamekosa lishe bora na kukabiliwa na tatizo la udumavu kwa zaidi ya wastani wa kitaifa ni Iringa, Njombe, Rukwa, Geita, Ruvuma, Kagera, Simiyu, Tabora, Katavi, Manyara, Songwe na Mbeya.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso