Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (Tanzania Footbal Federation (TFF) Kwa kushirikiana na uongozi wa Chama Cha Mpira wa miguu Wilayani Kahama KDFA mkoani Shinyanga wamezindua Rasmi mafunzo kwa walimu wa michezo wa shule za msingi na sekondari ikiwa ni pamoja na walimu wa team mbalimbali (Makocha) ambapo makocha 30 wanashiriki mafunzo haya
Akizungumza katika ufunguzi wa Mafunzo hayo Inspector Dismass Kifunda ambaye ni makamu Mkuu wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Kahama akimuakilisha Mkuu wa Jeshi la polisi Wilayani humo amesema kuwa michezo katika jamii inawasaidia wananchi katika mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupunguza uharifu katika jamii
Kwa upande wake mkufunzi wa mafunzo haya kutoka TFF Raymond Gweba amesema kuwa TFF wanalenga kukuza vipaji vya wanafunzi kupitia walimu wa michezo katika ngazi zote wakianza na miaka 3- 14
Mwenyekiti wa Chama Cha mpira wa miguu Kahama Hussein Salum amesema kuwa kuwepo kwa mafunzo hayo kutawapunguzia adha ambayo walikuwa wakikumbana nayo ya ukosefu wa walimu wa michezo wenye taaluma hali itakayokuza soka la Kahama
Kwa upande wao baadhi ya walimu waliohudhuria Mafunzo hayo akiwemo Hamad Sulle na Mwana Hamis Miraji wamesema kuwa kutokana na mafunzo haya wanatarajia kuboresha utendaji kazi wao katika kufundisha mpira kwani walikuwa wakifundisha pasina taaruma yoyote ya darasani
No comments:
Post a Comment