Maafisa wanaotekekeza Mradi wa Kuboresha Usimamizi wa Maliasili na Kukuza Utalii Kusini mwa Tanzania REGROW wamesisitizwa kuendelea kuteleza majukumu yao kwa kufuta kanuni taratibu, sheria na haki za binadamu ili kuufikisha mradi kwenye malengo yaliyokusudiwa.
Wito huo umetolewa Mkoani Morogoro na Msimamizi wa Mradi wa REGROW Dkt. Aenea Saanya alipokuwa akifunga Mafunzo maalum ya siku tano kwa Wataalam wanaotekeleza mradi huo, yaliyolenga kuwajengea uwezo katika nyanja ya Usimamizi na Uratibu wa Mikataba na Ununuzi katika Mradi huo unaotekelezwa kwa fedha za mkopo wa masharti nafuu kutoka Benki ya Dunia.
Dkt. Saanya ameongeza kuwa Wizara kupitia mradi wa REGROW imeona umuhimu wa kuendesha Mafunzo hayo ili kuimarisha uwezo wa Wataalam wanao tekeleza Mradi, wa kubaini viashiria vya changamoto kwenye Mikataba na ununuzi pamoja na kuzishughulikia maramoja kabla ya kusababisha athari kwenye utekelezaji wa mradi unaoendelea sasa.
Akizungumza kwa niaba ya washiriki wa Mafunzo hayo, Bi. Blanka Tengia, ameishukuru Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kuona umuhimu mkubwa wa kuwajengea uwezo wataalam wanotekeleza mradi na kuwa, taaluma waliyoipata watakwenda kuitumia kikamilifu katika kuhakikisha Malengo ya mradi yanafikiwa kupitia Ununuzi na Ugavi kwa maslami mapana ya Taifa.
Mradi wa REGROW unaotekelezwa kwa usimamizi wa Wizara ya Maliasili na Utalii, hadi sana umekuwa chachu kubwa ya maendeleo ya Uhifadhi na Utalii pamoja na maendeleo ya wananchi waishio pambezoni mwa Hifadhi za Taifa Mikumi, Nyerere, Udzungwa, Ruaha na Taifa kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment