KIONGOZI wa Mwenge wa Uhuru Kitaifa Godfrey Mnzava ameridhishwa na utekelezaji wa mradi wa kuboresha hali ya upatikanaji wa huduma ya maji Kata ya Chongoleani Jijini Tanga unaofanywa na mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga Uwasa).
Mradi huo pia utahusisha kata za Mabokweni na Mzizima Jijini Tanga zenye mitaa 10 na wakazi wapatao 26,071 ambapo miundombinu inayojengwa katika mradi huo inakusudia kuboresha hali ya upatikanaji wa huduma kwa wakazi wa maeneo hayo na hivyo kupata maji kwa kila siku kwa saa 24.
Lakini pia ikiwagusa watumiaji wengine ikiwemo wa viwanda,biashara pamoja na kampuni inayohusika na ulazaji wa bomba ka mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani Jijini Tanga nchini Tanzania.
Akizungumza mara baada ya kukagua mradi huo na kuuzindua ,Mnzava alisema wameridhishwa na mradi huo wa Tanga Uwasa kutokana na kwamba wao wamekuwa wakitekeleza maelekezo ya Serikali ya kutangaza miradi yote na zabuni kwenye mfumo wa kidigitali wa zabuni (NEST).
Alisema kwamba wanaendelea kuelekeza na kusisitiza hilo na ndio maelekezo ya Serikali miradi yote ya maendeleo ikiwa ni fedha kutoka Serikali kuu,wahisani,wadau wa maendeleo,mchango wa wananchi hata kama ni mapato ya ndani ya taasisi husika kama ni halmashauri na wakala wa serikali maelekezo kupitia sheria za kudhibiti matumizi ya fedha kwenye ununuzi wa umma yanawaelekeza takwimu zote zifanyike zipitia kwenye mfumo huo.
Alisema kwamba walikuwa na Tanel sasa wapo kwenye NEST lengo kubwa likiwa ni kudhibiti namna ya utoaji wa tenda ambapo mfumo huo umetengenezwa vizuri jinsi unavyoingia unakuchagua unakidhi vigezo vya kupata zabuni au haukidhi hautapata zabuni na hivyo kuondoa malalamiko na manunguniko.
Aidha alisema pia lakini hakuna upendeleo kwa hiyo katika utekelezaji wa mradi huo wamefanya hivyo niendelee kusisitiza ujumbe ufike kote nchini lazima waende kwenye mfumo wa Nest kwa sababu ndio mfumo waliopewa kwa sababu ya manunuzi ya umma kazi nzuri ya utekeleza wa mradi na mwenge wa uhuru upo tayari kufungua.
Awali akizungumza wakati akitoa taarifa ya mradi huo,Mhandisi wa Miradi wa Tanga Uwasa Mhandisi Violeth Kazumba alisema utekelezaji wa mradi huo ulianza mwezi Novemba mwaka 2022 ambapo ujenzi wake umefanywa na Mkandarasi M/S Engineerin Plus wa Jijini Dar es Salaam.
Mhandisi Kazumba alisema kwamba mradi huo wa uboreshaji wa hali ya upatikanaji wa huduma ya maji kata ya Mzizima,Mabokweni na Chongoleani umefadhiliwa na Taasisi inayohusika na ulazaji wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani Tanzania.
Ambapo usanifu wake umekadiriwa kugharimu kiasi cha sh.Bilioni 2,352,201,500 na hadi sasa mkandarasi amekwisha kulipwa kiasi cha fedha taslimu sh.Bilioni 1,823,766,540 sawa na asilimia 79.46.
Alisema mradi huo umekamilika mwishoni mwa mwezi Machi mwaka huu kwa asilimia 100 na hadi sasa unatoa huduma kwa jamii na mamlaka hiyo inaendelea kufanya maunganisho ya maji kwenye matawi pamoja na kwa watu binafsi kwa mujibu wa maombi yanayopokelewa kutoka kwa wahitaji.
“Ujenzi wa mradi huu ulihusisha ununuzi na ulazaji wa mabomba (kipenyo cha 315mm, 250mm,200mm,150mm na 110mm) kwa urefu wa mita 24,000,ununuzi na ufungaji wa viungio vya mabomba,ujenzi wa chemba 54 na usimikaji wa alama 309 za kuonesha njia aya mabomba”Alisema.
Akizungumzia faida za mradi huo Mhandisi Kazumba alisema kwamba utawezesha wakazi wa Kata ya Mzizima,Mabokweni na Chongoleani kupata huduma ya maji safi kila siku kwa saa 24 na itawezesha uwekezaji zaidi katika eneo hilo ikiwa ni pamoja na wawekezaji wa Bomba la mafuta ghafi (EACOP).
chanzo; Malunde1blog
No comments:
Post a Comment