BENKI ya CRDB imekabidhi Darasa la kisasa na Madawati 20 katika Shule ya Msingi Kiloleli wilayani Kishapu, ikiwa ni Sehemu ya kurudisha faida wanayoipata kwa jamii.
Makabidhiano hayo yamefanyika Aprili 9,2024 Shuleni hapo kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga AnaMringi Macha, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali na Chama pamoja na Wananchi wa Kijiji cha Kiloleli.
Mkuu wa Kitengo cha Malipo kutoka CRDB Madaha Chabba akizungumza kwenye hafla hiyo kwa niamba ya Mkurugenzi Mkuu wa CRDB, amesema utoaji mchango wa darasa hilo na Madawati 20 ni sehemu ya faida asilimia Moja ambayo hua wanaitoka kila mwaka kurudisha kwa jamii.
Chabba amesema yeye ni mzaliwa katika Kijiji hicho cha Kiloleli na amesema Shule ya Msingi Kiloleli Mwaka 1979 na amemaliza Darasa la Saba Mwaka 1985, na kwamba kutokana na uhaba wa Madarasa uliopo Shuleni hapo, aliuguswa na kuwasilisha Maombi kwa uongozi wa CRDB na kusaidia ujenzi wa Darasa na Madawati 20.
"Mimi ni Mzaliwa wa hapa Kiloleli nashukuru Benki ya CRDB ambayo naifanyia kazi kwa kukubali Ombi langu na kujenga Darasa hili likiwa na Madawati 20 ambayo yatakaliwa na wanafunzi 60," amesema Chabba.
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Jumanne Wagana,amesema kwamba Benki hiyo ilitoa kiasi cha fedha Sh.milioni 20 ili kufanikisha ujenzi wa Darasa hilo na baada ya chenji kubaki watatengeza na Madawati 20 na sasa darasa lipo tayari kutumiwa na Wanafunzi.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude,ameshukuru Benki hiyo kwa kuendelea kushirikiana nayo katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo, na kwamba Serikali itaendelea kuwa nao bega kwa bega.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha, ameipongeza Benki ya CRDB kwa kurudisha faida kwa jamii, na kujenga Darasa hilo na kutoa Madawati 20 huku akisisitiza litunzwe na kutoharibiwa miundombinu yake.
Amesema Serikali itaendelea kushirikiana na wadau katika Nyanja Mbalimbali za kimaendeleo ikiwamo Benki hiyo ya CRDB ambayo imekuwa na Mchango Mkubwa Serikalini katika kuwahudumia Wananchi.
Aidha, Macha ametoa wito kwa Wasomi ambao wamepita kwenye Shule hiyo ya Kiloleli kwamba wajitokeze ili kuendelea kutatua Changamoto ambazo bado zinaikabili ikiwamo ujenzi wa nyumba vya Madarasa.
Amesema kwa ujenzi wa vyumba Vitatu vya Madarasa shuleni hapo ambao umesimamia,ameitaka Serikali ya Kijiji kwamba waitishe Mkutano wa Kijiji ili kuendeleza ujenzi huo hadi hatua ya Renta na kisha yeye atachangia Mabati huku miundombinu mingine ikimaliziwa na Serikali.
Katika hatua nyingine,ametoa wito kwa wazazi kuendelea kusomesha watoto wao,pamoja na kuwatumizia Mahitaji ya shule ikiwamo kuwanunulia sare za Shule,huku akiwasisitiza wanafunzi wasome kwa bidii na kutimiza ndoto zao, ikiwamo kuiga Mfano wa Madaha Chabba ambaye amesoma Shuleni hapo, na sasa ni Mkuu wa Kitengo cha Malipo kutoka CRDB Makao Makuu.
Nao wanafunzi wa shule hiyo wameishukuru Benki ya CRDB kwa kuwajengea Darasa hilo pamoja na kuwapatia Madawati 20 huku wakiahidi kusoma kwa bidii na kutimiza ndoto zao.
No comments:
Post a Comment