Aliyekuwa baba Askofu wa kanisa takatifu katoliki la Orthodox Askofu Dkt. Francis Laurent Bukombe amesimikwa rasmi kuwa Askofu Mkuu wa kanisa hilo Tanzania.
Sherehe hiyo ya kusimikwa Uaskofu imefanyika leo Aprili 27, 2024 imeambatana na uzinduzi wa jengo la kanisa takatifu katoliki la Orthodox lililopo Kata ya Masekelo Manispaa ya Shinyanga.
Awali akizungumza wakati wa zoezi hilo Askofu Mkuu wa kanisa katoliki la Orthodox Askofu Mkuu Dkt. George Jamba amemsihi kuendelea kutoa huduma kwa watu wa aina zote bila upendeleo .
"Leo hii nimepokea jukumu hili naahidi kutumikia vyema kama vile MUNGU atakavyoniongoza, nishukuru sana wa wale wote waliojitokeza siku ya leo kushuhudia yale yaliyotendeka katika madhabahu hii, niwaombe tuendelee kushirikiana, mimi kama kiongozi wa kanisa hili niseme tu tutaendelea kushirikiana na serikali katika kukemea na kutokomeza matukio na vitendo vya ukatili kwenye jamii, ubakaji na ulawiti nitasimama kwa nguvu zangu zote kama Askofu kupinga vitendo hivyo”, amesema Askofu Dkt. Francis Laurent Bukombe.
“Nitapinga ukatili kwa watoto vipigo na udhalilishaji kanisa litaendelea kupinga na kuhakikisha malezi bora kwa watoto na jamii kwa ujumla, lakini pia hatutakuwa tayari kubariki ndoa ya jinsia moja, kanisa letu linapinga kwa nguvu zote ndoa ya jinsia moja kama Askofu sitakubali vitu vya namna hiyo”, ameongeza Askofu Dkt. Francis Laulent Bukombe.
Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye ulemavu ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi amempongeza Askofu Francis Laurent Bukombe kwa kusimikwa kuwa Askofu wa kanisa hilo.
“Hongera sana kwa mambo makubwa ambayo yametendeka kaika madhabahu hii, matunda uliyoyazaa ni ushuhuda wa watu uliyowaita hapa, mengi ulikumbana nayo lakini leo MUNGU amekuinua na kukuchagua wewe kuongoza kanisa hili, ulipo na imani kwa neno litakuwa”, amesema Mhe. Katambi.
Muonekano wa Kanisa takatifu katoliki la Orthodox lililopo kata ya Masekelo manisapaa ya Shinyanga.
Muonekano wa Kanisa takatifu katoliki la Orthodox lililopo kata ya Masekelo manisapaa ya Shinyanga.
Muonekano wa Kanisa takatifu katoliki la Orthodox lililopo kata ya Masekelo manisapaa ya Shinyanga.
No comments:
Post a Comment