Zoezi la ubomoaji wa nyumba zilizofidiwa na Mradi wa Uendelezaji wa Bonde la Msimbazi linatarajiwa kuanza rasmi Aprili 12, 2024, na litawahusu waathirika 2,155 ambao tayari wamelipwa fidia
Mhandisi Humphrey Kanyenye, Mratibu wa Miradi ya Ushirikiano na Benki ya Dunia TARURA
Hayo yamesemwa Machi 25 2024 na Mhandisi Humphrey Kanyenye, Mratibu wa Miradi ya Ushirikiano na Benki ya Dunia TARURA alipokuwa akiongea na waandishi wa habari katika ofisi za mradi zilizopo Millenium Tower-Kijitonyama, jijjni Dar es Salaam.
Mhadisi
Kanyenye ameeleza kuwa kwa mujibu wa makubaliano ya utekelezaji wa zoezi hilo,
waathirika wa mradi ambao wameshakwishapokea malipo yao wanatakiwa kuhamisha
mali zao na kupisha eneo la mradi ndani ya wiki sita (6) baada ya kupokea fedha
hizo kwenye akaunti zao.
“Waathrika
wote wa mradi huu wanafahamu kuwa tuliwapa muda wa kuhama kwa makubaliano
maalumu ya kimkataba yaliyowataka kuhama ndani ya wiki Sita (6) mara tu baada
ya fedha kuingia katika akaunti zao, muda huo sasa umepita hivyo wanatakiwa
kuondoka ili kupisha utekelezaji wa mradi,” amesema Mhandisi Kanyenye.
Ameeleza
pia kuwa walichelewa kuanza zoezi hilo kwa ajili ya kuwapa muda waathirika wa
mradi kubomoa wenyewe kwa hiari ili kuokoa baadhi ya mali zao.
Aidha,
amesema kwamba kati ya waathirika 2,329 waliopo kwenye orodha ya daftari la
kwanza la ulipaji fidia, kufikia tarehe 21 Machi 2024, tayari waathirika 2,151
walikuwa wamelipwa kiasi cha shilingi bilioni 52.6
“Lakini
pia kuna wale ambao hawakufikiwa katika uthamini wa awali kwa baadhi yao
kugomea ama kutoonekana katika maeneo yao, idadi yao ni 466, hawa wameingizwa
katika orodha ya daftari la pili ambalo limeshakamilika na litawasilishwa kwa
Mthamini Mkuu wa Serikali kwa ajili ya kusainiwa siku ya jumanne tarehe 26
Machi 2024 tayari kwa kulipwa fidia,” amesema Mhandisi Kanyeye.
Mradi unatekelezwa kwa muda wa miaka
sita (6), 2022-2028 kwa gharama takribani shilingi bilioni 663 na lengo
kuu la mradi ni kuimarisha ustahimilivu kwa kuweka mikakati ya kukabiliana na
mafuriko na kuwa na matumizi bora ya ardhi katika eneo la chini la bonde la mto
msimbazi ikiwa ni pamoja na kurudisha uoto wa asili katika uwanda wa juu wa
bonde la mto msimbazi.
No comments:
Post a Comment