Zaidi ya wananchi 300 wa Kata ya Kashenye na wenzao kutoka kata jirani ya Kanyigo, ambao Mama zao au Bibi wanatoka wilaya za Ngara na Biharamulo tarehe 02 Machi 2024, wamejumuika pamoja katani Kashenye, katika jitihada za kuimarisha umoja who, ikiwa ni pamoja na kuishinisha michango katika mfuko wa umoja huo.
Mkutano huo umefanyika ukumbi wa Kyaishozi katika senta ya kijiji Bukwali, ukifunguliwa na mwenyekiti wa umoja huo katika kata ya Kashenye, Joas Mbanga.
NA MUTAYOBA ARBOGAST, HUHESO DIGITAL, BUKOBA
Akizungumza katika mkutano huo, mratibu wa umoja huo maarufu kama Abalumuna, Gaspar Rutalugamubyemo Mikimba, amesema,"Sisi watoto ambao mama zetu wanatoka Ngara na Biharamulo, hakika tunazo sababu za kumshukuru sana Mwenyezi Mungu aliyetuumba na kwa zawadi aliyotupa ya damu za Mama,Bibi zetu au Baba zetu kutoka Buhangaza,Bushubi na Buzinza. Hivyo sisi tulioko ndani ya kundi hili Ngara au Biharamulo ni ujombani"
Ameyataja malengo ya muda mfupi na mrefu kuwa ni pamoja na upendo,umoja na kwa kujaliana, na hivyo kinda mfuko wa umoja huu utakaosaidia kwa shida na raha, Bima ya Afya, Elimu, hata kuyatibu safari za kutembelea ujombani kadri hali itakavyoruhusu.
Wajumbe wote kwa pamoja wamekubaliana kutoa michango yao kwa kuanzia na sh 20,000 hadi mwishoni mwa Aprili, na baadaye sh 2,000 kila mwezi huku huduma za mwanzo zikisubiri kipindi cha mpito.
Nickson Rutagwerela wa kijiji cha Kashenye amesisitiza umuhimu wa suala la musimamizi wa fedha,ili makosa yanayofanyika au yaliyofanyika nyuma kwa baadhi ya SACCOS na vyama vya kijamii yasije kujitokeza katika umoja huo.
Bibi Johana Miburo(78) ambaye ameonesha furaha kuu kipindi chores cha mkutano amesema furaha yake imetoka na kuona anakutana na ndugu wenye asili moja ambao kabla hakuwajua licha ya kuwa wamekuwa kukutana nao.
"Nilizaliwa kijiji Kashange, kata Kilusha wakati wauongozi wa Balamba.Nilimfuata dada nikaolewa huku, namshukuru Mungu nina watoto na wajukuu", amesema Bibi huyo huku alisema atatoa michango yake kwa wakati, na atakuwa mstari wa mbele kutembelea ujombani Ngara.
Kikundi cha baadhi ya wanawake kutoka kijiji cha Bukwali, wamemetoa zawadi mbalimbali kwa mratibu wa umoja huo, wakisema siku nyingi wamekuwa na wazo kama hilo, lakini hawakuwa na utayari na uwezo wa kuanzisha umoja.
Mkutano kama huo ulifanyika katani Kanyigo tarehe 03 Februari mwaka huu, na umepangwa kufanyika tena tarehe 04 Mei katika kata ya Kanyigo.
No comments:
Post a Comment