Waziri wa madini Antony Mavunde (mb) amezindua kituo cha mafunzo cha Barrick Academy wilayani Kahama mkoani shinyanga chenye malengo ya kuongeza ubunifu na ujuzi wa wataalam katika sekta ya madini nchini.
NA NEEMA NKUMBI-KAHAMA
Kituo hicho ambacho kipo ulipokuwa mgodi wa madini Buzwagi ambao umefungwa kutokana na kumaliza ushalishaji wa uchimbaji madini ya dhahabu, Waziri mavunde akiwa mgeni rasmi amesema kituo hicho cha mafunzo kitakuwa chachu ya kuongeza wataalam wa madini nchini.
Mavunde amesema kuwa kuwepo kwa kituo hicho ni dhamira ya dhati ya kampuni ya ucimbaji madini aina ya dhahabu Barrick katika kuwaendeleza watu mbalimbali kupata ujuzi ili kuendana na Sayansi na teknorojia katika sekta ya madini nchini ambapo watu wanaotarajiwa kupatiwa mafunzo ni 1024 kwa mwaka 2024.
Aidha baadhi ya kozi ambazo zitatolewa ni Pamoja na masuala ya usalama, utoaji wa uamzi na usuluhishi wa migogoro na usimamizi wa gharama katika miradi mbalimbali ambayo Waziri Mavunde amesema hiyo itasaidia kuongeza uelewa wa watu.
Waziri Mavunde ameongeza kuwa eneo hilo la Buzwagi ni moja ya maeneo machache ambayo yanatarajiwa kuleta mabadiliko ya kweli kwenye sekta ya madini huku akisema wao kama serikali wanayo mipango na mikakati ya kuhakikisha sekta ya madini inaendelea kulinufaisha taifa na mchango wa sekta ya madini umeendelea kukua.
Amesema kuwa eneo la Buzwagi litakuwa sehemu ya kutoa mchango mkubwa nchini katika sekta ya madini kwenye kusaidia kuongeza thamani ya madini na kutoa huduma katika migodi mingi huku akisema Mhe. Rais Samia katika maelekezo yake ni kuhakikisha thamani ya madini nchini inaongezeka.
Waziri wa madini Antony Mavunde akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo cha mafunzo Barrick Academy
Nae mbunge wa jimbo la Kahama mjini Jumanne Kishimba ameiomba kampuni ya Barrick kuhakikisha katika kituo hicho cha mafunzo cha Barrick Academy kuwasaidia wachimbaji wadogo wilayani Kahama ili kuwapatia ujuzi utakaosaidia ubunifu zaidi kwenye shughuli zao.
Kwa upande wake afisa mkuu wa uendeshaji wa Barrick katika kanda ya Afrika na Mashariki na kati, Sebastian Bock amesema kuwa kituo hicho kitakuwa kinatoa mafunzo kwa watu wote licha ya kipaumbele cha watanzania pia watakuwepo watu ambao watakuwa wanapatiwa mafunzo kutoka nje ya Tanzania kwa miaka miwili na watakaopatiwa mafunzo hayo ni zaidi ya watu 2000.
No comments:
Post a Comment