Serikali kupitia Wizara afya imepokea vidonge vya matone ya Vitamini A milioni 22 kutoka kwa shirika la Nutritrion International kwa ajili ya kuwapatie watoto walio na umri chini ya miaka 5 wapatao milioni 11 kwa ajili ya kuongeza kinga ya mwili na kuimarisha afya ya macho kwa watoto hao.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya Dk. Godwin Mollel Machi 13, 2024 wakati wa makabidhiano ya vidonge vya matone ya Vitamini A kutoka shirika la Nutrition International NI jijini Dar Es Salaam.
Dkt. Mollel amesema Vidonge vya matone ya Vitamini A vitasaidia kuongeza kinga ya Mwili na kuimarisha afya ya macho kwa watoto walio na umri chini ya miaka tano.
Dkt. Mollel amewataka watanzania kuzingatia milo yao ya kila siku kwa kupata chakula chenye lishe hasa vyenye vitamini ili kuepugana na magonjwa yasiyoambukiza kama shinikizo la damu , magonjwa ya moyo na kisukari
Kwa upande wake Rais Mstaafu wa awamu ya Nne, Dk. Jakaya kikwete ambae pia ni mjumbe wa bodi ya menejimenti nchini ya shirika la Nutrition International (NI) amesema shirika la Nutrition Internation limepatia Serikali vidonge vya matone vya Vitamini A milioni 22 kwa mwaka 22 na kuongeza kuwa vitamini A umsaidia mtoto kuimarisha afya ya macho na kuongeza kinga mwinili.
No comments:
Post a Comment