WATOTO 8 WAMEFARIKI NA WATU WENGINE ZAIDI YA 70 WAMELAZWA WAKIDHANIWA KULA SAMAKI ZANZIBAR - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday 8 March 2024

WATOTO 8 WAMEFARIKI NA WATU WENGINE ZAIDI YA 70 WAMELAZWA WAKIDHANIWA KULA SAMAKI ZANZIBAR

Watoto wanane wamefariki dunia na watu wengine 78 wamelazwa hospitali kwa madai ya kula samaki aina ya kasa kisiwani Panza, Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba.


Hata hivyo, Daktari wa Wilaya ya Mkoani, Haji Bakari Haji alisema jana kuwa, awali alipowauliza wagonjwa kinachowasibu hawakuweka wazi, hivyo walichukua sampuli na kuzipeleka maabara kwa ajili ya uchunguzi zaidi kufahamu chanzo cha tatizo hilo.


Alisema jumla ya wagonjwa 86 waliofikishwa hospitali wanane wamepoteza maisha.


Dk Haji alisema tukio hilo lilitokea Machi 5 mwaka huu kisiwani hapo.


Soma kwa undani www.mwananchi.co.tz

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso