“Tunatengeneza vikapu lakini pia mizinga tunayopalepale Udiakonia na tunapata asali mbichi,sisi kwenye kundi letu tuna viziwi ambao ndio wanaohusika kuweka mizinga na kupaka nta ila kwenye masoko yetu asali sio tatizo sana kwasababu watu wanajua umuhimu wake lakini vikapu soko bado”amesema Hekima
Naye mwenyekiti wa UWT mkoa wa Njombe amesema walemavu wamekuwa na mchango mkubwa kwenye maendeleo kwa kutengeneza bidhaa mbalimbali na kufanya shughuli kama watu wengine hivyo kuna umuhimu mkubwa kuuungwa mkono huku akiahidi kufikisha kwenye serikali changamoto za wanawake hao ili ziweze kufanyiwa kazi.
“Kina mama wenzetu hawa wanafanya kazi kubwa lazima tuwaunge mkono,niombe jamii iione changamoto hii na wadau mbalimbali waendelee kuwaona watu hawa na sisi kwa nafasi zetu lazima tuwasaidie”amesema Scolastika Kevela
Aidha katika kuadhimisha siku hiyo ya wanawake,Mwenyekiti kwa kushirikiana na wanawake wilayani Makete wamefanikiwa kutembelea na kuwaona wafungwa na Mahabusu walioko kwenye gereza la Ndulamo na kukabidhi mahitaji mbalimbali pamoja na kutoa taulo za kike kwa wanafunzi wa Sekondari ya Ilumaki
No comments:
Post a Comment