Bodi ya wakurugenzi Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) ikiongozwa na Mwenyekiti wake Meja Jenerali (mstaafu) Hamis Semfuko imefanya ziara ya siku moja ya kutembelea mapori ya akiba ya Ikorongo na Grumet yaliyopo katika Wilaya ya Serengeti mkoani Mara.
Akizungumza na maofisa na askari wa mamlaka hiyo eneo la Fort Ikoma, Mwenyekiti wa bodi hiyo alisisitiza nidhamu kwa maofisa na askari wa mamlaka hiyo katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku hasa shughuli za uhifadhi.
Mbali na nidhamu Meja mstaafu Semfuko alisisitiza zaidi uwepo wa ushirikiano kati ya mamlaka hiyo pamoja na wawekezaji ikiwemo Kampuni ya Grumet Fund Trust katika kuhakisha shughuli za uhifadhi zinahimarishwa.
Mwenyekiti huyo alibainisha kuwa askari na maofisa wa mamlaka hiyo kipaumbele chao cha kwanza katika utendaji kazi wao inatakiwa kuwa ni nidhamu, ikiwa pamoja na kufanya kazi kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa.
Alisema kuwa Bodi kwa ushirikiana na serikali wameendelea kufanya maboresho makubwa ndani ya mamlaka hiyo, kwa kuboresha mazingira ya utendaji kazi wa watumishi hasa kuongeza vitendea kazi.
No comments:
Post a Comment