Akitoa suluhisho la kudumu kutokana na mtifuano huo kati ya NHIF na watoa huduma binafsi, Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) Dk Baghayo Saqware akizungumzia kwa upande wa huduma za dawa, amesema kinachotakiwa ni uwepo wa mwongozo wa bei.
“Wakati wa kamati ya kitita kipya nikiwa kama Mwenyekiti wa kamati hiyo tuliongea na NHIF watoa huduma na wadau wengine, tukapata mapendekezo yao, tukagundua kuna mambo yanachanganywa mfano tunasahau kuwa masuala ya NHIF na watoa huduma ni masuala ya kimkataba.
“Kwenye suala la bei lazima kuwe na mfumo wa mapendekezo ili mfuko ulipe. Kama kamati tukakubaliana na tukaona suluhisho la kudumu katka kitita hichi ni kuwa na bei elekezi ya ununuzi, uwiano wa faida na gharama za usimamizi ambazo ni vigezo vya kisayansi na kibiashara.
Amesema hayo wakati akichangia mada leo Machi 6, 2024 kwenye mjadala wa Mwananchi X Space ulioandaliwa na Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd wenye mada isemayo; Nini kifanyike kupata suluhisho la kudumu baina ya NHIF na watoa huduma binafsi?
No comments:
Post a Comment