RAIS YOWERI MUSEVENI AMTEUA MTOTO WAKE KUWA MKUU WA MAJESHI YA ULINZI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Saturday, 23 March 2024

RAIS YOWERI MUSEVENI AMTEUA MTOTO WAKE KUWA MKUU WA MAJESHI YA ULINZI

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, amemteua mtoto wake, Jenerali Muhoozi Kainerugaba kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF).Gazeti la Daily Monitor la Uganda limeripoti.

Anachukua nafasi ya Jenerali Wilson Mbasu Mbadi ambaye ameteuliwa kuwa Waziri wa biashara katika mabadiliko mapya ya safu ya Baraza la mawaziri lililotangazwa karibuni.


Jenerali Muhoozi alikuwa akihudumu nafasi ya mshauri mkuu wa Rais katika masuala ya operesheni maalumu.



Mamlaka ya mkuu wa majeshi yalifanyiwa mageuzi na kutangazwa mwezi uliopita wa Februari. Kwa baadhi ya wadadisi na wanasiasa, uteuzi wa Jenerali Muhoozi kuwa mkuu wa majeshi ulipangwa tangu zamani.


Kwa hiyo si ajabu kwamba sasa umehalisika katika kipindi kuelekea msimu wa uchaguzi mkuu. Kiongozi wa upinzani Dkt Kizza Besigye amesema kwamba "nchi hii ilikwisha tekwa serikali sasa imetekwa kwani hata majeshi yametekwa na familia".


Kwa upande mwingine, kuna mtazamo kuwa sasa Museveni amemdhibiti vilivyo mwanawe ambaye alikuwa ametangaza kugombea urais na kuzindua vuguvugu la kumpigia debe.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso