Mwili wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Pili wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi, unatarajiwa kuzikwa tarehe 2 Machi 2024, mjini Unguja.
Ratiba ya mazishi ya marehemu Mwinyi imetangazwa 29 Februari 2024 na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, wakati akitangaza kifo chake.
“Kwa niaba ya Serikali ninatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na Watanzania wote kwa msiba huu mkubwa kwa Taifa letu. Nchi yetu itakuwa katika kipindi cha siku saba za maombolezo, ambapo bendera zitapepea nusu mlingoti kuanzia Machi 1, 2024, Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi atazikwa tarehe 2 Machi 2024 huko Unguja, kisiwani Zanzibar ,” Amesema Rais Samia
“Inna Lillahi wa inna ilayhi raaji’un.”
Rais Mwinyi, amefariki dunia Ijumaa Februari 29, 2024 majira ya saa 11:30 jioni, katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Emilio Mzena, Dar es Salaam, alipokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa Saratani ya Mapafu.
Ali Hassan Mwinyi alikuwa Rais wa awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia mwaka 1985 hadi 1995.
No comments:
Post a Comment