Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoani Shinyanga Mabala Mlolwa ameitaka Halmashauri ya Msalala Wilayani Kahama Kuhakikikisha inarejesha kiasi cha Sh,Milioni 16 wanazirejesha kwa wanufaika wa mfuko wa TASAF kwenye Halmashauri hiyo.
Mwenyekiti wa CCM Mabala Mlolwa ameoneshwa kuchukizwa na kitendo kilichofanywa na watumishi wa Halmashauri hiyo kwa kutafuna fedha za wanufaika wa mfuko wa maendelo ya jamii TASAF jambo ambalo ni kinyume cha Sheria.
“Kusimamishwa watumishi sio kigezo tunachotaka ni pesa irudishwe yani kweli unakula pesa ya mtu masikini uoni hata aibu kabisa harafu Kaimu Mkurugenzi unakuja unatuambia eti umewasimamisha watumishi hii kauli sikubaliani nayo Mpigie simu Mkurugenzi mtendaji wa Msalala Mwambie Mwenyekiti anataka pesa ya wanufaika wa TASAF ilipwe sikubali kuona uonevu wa kwa wananchi” amesema Mabala
“Ndugu Mwenyekiti nikuhakikishie kuwa kiasi cha Milioni 16 ambazo zimebakia tutahakikisha tunazirudisha kwa wakati kwa wanufaika wa mfuko wa TASAF tunaomba mtusamehe tu kwani tayari tunaendelea na mchakato wa Malipo ya Fedha zote zinazodaiwa” amesema Mfilinge Abdulllah, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Msalala, Mibako Mabubu amemuhakikishia Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Kuhakikisha ifikapo Ijumaa ya wiki hii pesa zote zitakuwa zimefika kwa walengwa.
Kwa upande wake Mbunge wa
Msalala Iddi kassim Iddi ameahidi kushughulika na watu
ambao wataonekana kudhurumu haki za wananchi.
Chanzo : FullShangwe
No comments:
Post a Comment