ACCRA, Ghana: Mashindano ya Afrika (All African Games 2023) yamezinduliwa rasmi Machi 8, 2024 jijini Accra, Ghana.
Rais wa Ghana, Nana Akufo Addo aliongoza uzinduzi wa michuano hiyo ,huku yakishuhudiwa na wanamichezo kutoka Mataifa 54 ikiwemo Tanzania na kupambwa na maandamano pamoja na burudani mbalimbali.
Mashindano hayo yanatarajiwa kuwa na washiriki zaidi ya 8000 wakijumuisha wachezaji, maofisa, madaktari wa timu pamoja washangiliaji ambapo michezo mbalimbali inatarajia kuchezwa katika viwanja tofauti kuanzia Machi 8 hadi 23, 2024.
Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Hamis Mwinjuma ameongoza timu ya wanamichezo kutoka Tanzania watakaochuana na wachezaji wa mataifa mengine katika mchezo wa kriketi wanawake, mpira wa miguu wanawake chini ya miaka 20, Judo, Riadha, kuendesha baiskeli na kuogelea.
No comments:
Post a Comment