WIZARA ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imewahimiza wadau wa somo la hisabati kuendelea kushirikiana na Serikali katika kutatua changamoto zinazolikabili somo hilo kwa wanafunzi ukiwemo uelewa mdogo na ufaulu mdogo.
Naibu Katibu Mkuu kutoka Wizara hiyo anayeshughulikia elimu Msingi, Dk Franklin Rwezimula, amesema hayo mjini Morogoro kwenye kilele cha Maadhimisho ya Tano ya Kitaifa ya siku ya Hisabati Duniani (IDM).
Maadhimisho ya mwaka huu yalibeba kauli mbiu "Cheza na Hisabati" na kuratibiwa na Chama Cha Hisabati Tanzania (MAT/CHAHITA).
No comments:
Post a Comment