WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ameongoza Mkutano wa Wabunge wote wa kupokea Mapendekezo ya Serikali ya Mpango na Kiwango cha Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka fedha 2024/2025.Mkutano huo umefanyika leo Machi 11, 2024 katika ukumbi wa Pius Msekwa jijini Dodoma.
Mapendekezo ya Serikali ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka wa fedha 2024/25 yaliwasilishwa na Waziri wa Ofisi ya Rais-Uwekezaji na Mipango, Profesa Kitila Mkumbo huku Mapendekezo ya Mfumo na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka fedha 2024/2025 yakiwasilishwa Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba.
Mara ya baada ya kuwasilishwa kwa Mapendekezo hayo, Naibu Spika wa Bunge, Mussa Azzan Zungu kwa niaba ya Spika amelekeza Kamati ya Kudumu ya Bajeti kuyafanyia kazi Mapendekezo hayo na kuzishauri Kamati za kisekta ipasavyo.
Kwa upande mwingine Wabunge ambao ni wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge takribani 14 wataanza kufanya ziara za ukaguzi wa miradi ya Maendeleo nchi nzima.
No comments:
Post a Comment