Imeelezwa kuwa, Tanzania inakabiliwa na changamoto mbili za ukuaji wa uchumi ikiwamo kushindwa kutafsiri namna ya kupunguza umaskini na tatizo la ongezeko la watu linalotokana na kuzaliana.
Hii ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Benki ya Dunia (WB).
Taarifa hiyo inasema wakati hali ya Pato la Taifa (GDP) ikitarajiwa kukua kwa asilimia 5.6 mwaka 2024 na fursa endelevu kwa karibu asilimia 6, Watanzania wengi bado wanakabiliwa na umaskini.
Benki hiyo imebainisha hayo jijini Dar es Salaam jana katika uzinduzi wa toleo la 20 la Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Tanzania.
Takwimu za benki hiyo ya dunia zinaonyesha karibu Watanzania milioni tatu wameingia kwenye umaskini wakati na baada ya mlipuko wa ugonjwa wa Uviko-19.
Inasema mwaka 2018, takriban Watanzania milioni 14 walikuwa wakiishi katika umaskini, lakini kufikia mwaka 2022, idadi hiyo iliongezeka hadi kufikia milioni 17.
No comments:
Post a Comment