ICC YATOA HATI KUKAMATWA MAKAMANDA WAKUU WA RUSSIA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday, 6 March 2024

ICC YATOA HATI KUKAMATWA MAKAMANDA WAKUU WA RUSSIA


Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) imetoa hati ya kukamatwa kwa makamanda wakuu wa Russia, kwa tuhuma za uhalifu wa kivita nchini Ukraine.





Imeandaliwa kwa msaada wa BBC

Miongoni mwa waliotajwa ni Luteni Jenerali wa Jeshi, Sergei Kobylash na Amiri wa Jeshi la Wanamaji, Viktor Sokolov.


Hii ni awamu ya pili ya kutolewa hati ya kukamatwa kwa maofisa wa Russia kuhusiana na vita nchini Ukraine.


Ya kwanza ilikuwa ya Rais, Vladimir Putin na mjumbe wake wa haki za watoto nchini humo.


Russia haiitambui Mahakama ya ICC, na hivyo kufanya kusiwe na uwezekano mkubwa wa kupelekwa kujibu mashtaka.


Taarifa ya ICC ilisema watuhumiwa hao wawili walihusika na mashambulio ya makombora yaliyofanywa na vikosi vilivyo chini ya amri yao, dhidi ya miundombinu ya umeme ya Ukraine.


Uhalifu wa Russia kwa Ukraine unadaiwa ulifanyika kati ya Oktoba 2022 na Machi 2023, huku ICC ikisema kuwa mashambulizi hayo yalisababisha madhara kwa raia.


Kobylash (58), alikuwa kamanda wa safari za anga za masafa marefu wa Jeshi la Anga la Russia wakati wa madai ya uhalifu. Sokolov (61), alikuwa kiongozi katika jeshi la wanamaji la Urusi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso