DOROTHY SEMU AMRITHI ZITTO - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday, 6 March 2024

DOROTHY SEMU AMRITHI ZITTO


Dorothy Semu amechaguliwa kuwa kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, akichukua nafasi ya Zitto Kabwe ambaye amemaliza muda wake wa uongozi kwa mujibu wa katiba ya chama. 





Katika kinyang’anyiro hicho, Semu ameshinda kwa kupata kura 534 sawa na asilimia 65.7 ya kura zote, huku mshindani wake, Mbarala Maharagande akipata kura 184 sawa na asilimia 34.3%.


Semu ana shahada ya pili ya sayansi ya tiba ya viungo (Physiotherapist) kutoka Chuo cha Western Cape, Afrika Kusini.


Alianza kazi mwaka 1998 kama mtumishi wa umma na ameitumikia serikali kwa miaka 17.


Aliingia rasmi kwenye ulingo wa siasa akiwa na umri wa miaka 40. Akiwa ACT Wazalendo, Semu alitumikia nyadhifa mbalimbali kama Katibu wa Sera na Utafiti, Katibu wa Fedha, Katibu Mkuu na Kaimu Mwenyekiti Taifa, Makamu Mwenyekiti na Waziri Mkuu Kivuli.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso