Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) inatarajiwa kujifungia kwa siku mbili kuanzia leo kuandaa Azimio la Mtwara la kushiriki au kutokushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka huu.
Pia, kikao hicho kitakachohitimishwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe kitafanya tathimini ya maandamano ya amani waliyoyafanya katika majiji ya Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya na Arusha.
Februari 27 mwaka huu, Mbowe akihutubia mamia ya wananchi viwanja vya Reli, Arusha katika maandamano ya amani alisema wanakwenda kujifungia mkoani Mtwara kufanya tathimini ya maandamano hayo na mikakati mingine ya chama.
Lengo la maandamano hayo yaliyopewa jina la ‘Vuguvugu la haki ya Watanzania’ ni kuishinikiza Serikali kushughulikia gharama za maisha kwa madai kuwa, yamekuwa magumu kutokana na mfumo wa bei za bidhaa mbalimbali.
Soma kwa undani www.mwananchi.co.tz
No comments:
Post a Comment