Serikali ya Kuwait imekuwa msaada kwa Serikali ya Tanzania katika Sekta ya Afya ambapo imeweza kusaidia mipango kadhaa ikiwa ni pamoja na kutoa msaada wa mashine za ganzi kwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu
Waziri
wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amesema hayo
usiku wa jana Februari 21, 2024 Jijini Dar Es Salaam kwenye Maadhimisho ya
Miaka 63 ya Uhuru na miaka 33 ya Siku ya Ukombozi wa Kuwait ambapo kwa Tanzania
Maadhimisho hayo yameongozwa na Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Mubarak Mohammad
Alsehaijan.
“Kwa
nafasi yangu kama Waziri wa Afya, kwa namna ya pekee kabisa napenda kuishukuru Serikali ya Kuwait kwa msaada
wake katika Sekta ya Afya pamoja na kutoa
msaada wa mashine za ganzi wameweza
kusaidia vifaa vya upasuaji kwa watoto wanaosumbuliwa na vichwa vikubwa
(Hydrocephalus) kwenda Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI).” Amesema Waziri Ummy
Mhe, Ummy Mwalimu na Balozi wa Kuwait Mhe. Mubarak Mohammad Alsehaijan.
Waziri
Ummy amesema Kuwait imesaidia pia kwa kutoa Vifaa Tiba
katika Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar, Mashine za Watoto Wachanga zisizo na
hewa kwa Hospitali ya Benjamin Mkapa mjini Dodoma pamoja na ujenzi wa Hospitali
ya Handeni Mkoani Tanga inayofadhiliwa na Taasisi ya Abdullah Al Nouri ya Kuwait.
Aidha,
kwa mwaka 2023 Kuwait
kupitia Kuwait Children Heart
Association ilileta madaktari bingwa walioshirikiana na watalaam wa Hospitali
ya Benjamin Mkapa Dodoma na kufanya upasuaji wa moyo bure kwa watoto 100 wa kipato cha chini Nchini.
“Hatua hizi zinaashiria
kwamba uhusiano wa kindugu na urafiki uliopo kati ya nchi zetu mbili (Tanzania
na Kuwait) nina imani kuwa uhusiano huu
utaendelea kuwa wa karibu na chini ya uongozi wa busara mahiri na mwanga wa viongozi wetu wawili, Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan na
Sheikh Mishal al-Ahmad al. -Sabah, Amir wa Kuwait.” Amesema Waziri Ummy
Chanzo : Fullshangwe
No comments:
Post a Comment