RAIS RUTO WA KENYA NA TUNUBU WA NIGERIA WAKOSOLEWA KUSAFIRI SANA NJE YA NCHI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday, 19 February 2024

RAIS RUTO WA KENYA NA TUNUBU WA NIGERIA WAKOSOLEWA KUSAFIRI SANA NJE YA NCHI


Rais William Ruto wa Kenya na Rais Bola Tinubu wa Nigeria, wanakabiliwa na ukosoaji kwa safari zao za mara kwa mara nje ya nchi.


Wawili hao wamekuwa wakikosolewa kutokana na gharama zinazohusiana na safari nyingi za ndege wakati kuna hali ngumu ya kiuchumi nyumbani.


Gazeti la Kenya, Standard, lilimtaja Ruto kuwa "Rais Anayepaa." Gazeti hilo limeandika "kupenda kwake kusafiri, anaonekana hawezi kuacha fursa yoyote" licha ya mahitaji makubwa ya nyumbani, kama vile kukabiliana na gharama ya juu ya maisha.


Mwezi uliopita, Tinubu alifanya safari nyingine barani Ulaya, kiongozi wa upinzani wa Nigeria Atiku Abubakar alisema kwenye mitandao ya kijamii, Nigeria haihitaji "mkuu wa utalii." Alikosoa ziara ya rais "wakati Nigeria inazama katika bahari ya ukosefu wa usalama."


Ni ukweli kuwa, Marais wanapaswa kuhudhuria mikutano ya wakuu wa nchi na kukuza uhusiano wa kigeni. Ni muhimu sio tu kwa sababu za kidiplomasia, lakini pia za kiuchumi, kwani mikataba yenye faida kubwa ya uwekezaji inaweza kujadiliwa.


Lakini baadhi wameeleza kuwa marehemu Rais wa Tanzania John Magufuli hakuwahi kusafiri nje ya Afrika katika miaka yake sita madarakani.

Habari zaidi tembelea

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso