Nyumba biashara na magari viliharibiwa huku video ikionyesha moto mkubwa ukiwaka karibu na majengo ya ghorofa. Hapo awali serikali imesema mlipuko huo umetokea katika kiwanda cha gesi chanzo cha moto huo bado hakijajulikana.
Msemaji wa
serikali Isaac Mwaura amesema eneo la mlipuko kwa sasa limezingirwa na kituo cha kuendesha
operesheni ya uokoaji kimeanzishwa kusaidia kuratibu shughuli za uokoaji.
"Wakenya
wameshauriwa kuepuka eneo lililozingirwa ili kuruhusu shughuli ya uokoaji
kutekelezwa bila usumbufu "amesema msemaji wa serikali
Moto huo
unaripotiwa kuenea katika majengo kadhaa ya ghorofa na kusababisha hofu
kutanda kwa wananchi wa eneo hilo na idadi ya waliojeruhiwa inaweza kuongezeka
zaidi.
Mmoja wa waliojeruhiwa Boniface Sifuna ameelezeea kilichotokea kwa shirika la habari
la Reuters: "Nilichomwa na mtungi wa gesi uliolipuka nilipokuwa nikijaribu
kujiokoa " alisema
Shahidi
ambaye jina lake halikutajwa amesema "milipuko mikubwa, mipira mikubwa ya
moto, watu kupiga mayowe na kukimbia kila mahali kwa kuhofia milipuko
zaidi".
Shirika la
Msalaba Mwekundu la Kenya limesema kwenye mitandao ya kijamii kwamba
wafanyakazi wamekuwa "wakipambana na moto huo bila kuchoka".
Chanzo: BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment