MAMIA WAMZIKA,WAOMBOLEZA KIFO CHA BALOZI DK KAMALA, AMEACHA ALAMA ZISIZOFUTIKA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday, 21 February 2024

MAMIA WAMZIKA,WAOMBOLEZA KIFO CHA BALOZI DK KAMALA, AMEACHA ALAMA ZISIZOFUTIKA


Mamia ya wananchi wilayani Missenyi na kwingineko, wamejitokeza kuomboleza na kuusitiri mwili wa Balozi, Dk Deodorus Buberwa Kamala, kijijini kwake Rwamashonga , kata ya Bwanjai, tarehe 20 Februari 2024, mazishi ambayo yameongozw na Katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi,Balozi,Dk Emmanuel Nchimbi.



Katibu mkuu wa CCM, Balozi Emnanuel Nchimbi(kushoto) na mkuu wa mkoa wa Kagera, Fatma Mwassa.


Na Mutayoba Arbogast, HUHESO DIGITAL Blog, Bukoba


Dk Kamala aliwahi kuwa mbunge wa jimbo la Nkenge mwaka 2000 hadi 2010, kisha mwaka 2015 hadi 2020.


Balozi Nchimbi alimueleza bakozi Kamala kuwa alikuwa mtu mnyenyekevu asiyependa makuu,aliyechukia rushwa, na aliyelitumikia taifa na watu wa jimbo lake kwa uadilifu na uaminifu na siyo kwa maslahi yake binafsi.


"Tunahitaji vionjozi wanaotanguliza maslaji ya umma ,wana Nkenge mshukuruni Mungu kwa kumpata kiongozi kama huyo,CCM tutaendelea kuwaenzi wabunge wote wanaofanya vizuri na tunajua na kutambua kuwa wajibu wetu wa kwanza ni kuwatumikia wananchi. Wapo viongozi wasiopenda rushwa na wanatumikia Taifa kwa nguvu zao zote katika kuwatetea na kuwalinda kwasababu wanatimiza wajibu wao kama inavyotakiwa na wale ambao bado wanasuasua wajitafakari", amesema Nchimbi.

Profesa Theobard Frank Theodori, aliyefadhiliwa  na  Kamala katika mapambano ya kusaka elimu


Mbunge wa jimbo la Nkenge, Florent Kyombo amesema tukio hilo ni zito na ni ngumu kuishi nalo kwa sababu marehemu Balozi Kamala aliishi vizuri na Wanamissenyi wenzake na pia katika kipindi chote cha ubunge wake aliishauri vizuri Serikali.


Naye mkuu wa mkoa wa Kagera Fatma Mwassa,mesema Missenyi ilijaliwa kuwa nambunge shupavu na ndiyo maana alichaguliwa kwa vipindi zaidi ya kimoja.


Akiongea kwa uchungu mkubwa mbele ya waombolezaji, Profesa Theobard Frank Theodori, Profesa mwenye umri mdogo kuliko wote Tanzania (42), amesema amefanikiwa mapambano ya kusaka elimu kutokana na ufadhili wa Dr Kamala kwani baada ya kufiwa na wazazi wake akiwa na umri mdogo, alichukuliwa kuwa miongoni mwa wanafamilia.


Mmoja wa watoto wa marehemu,Catherine Kamala, amemueleza baba yao kuwa alikuwa nguzo muhimu katia familia aliwajali na kuwatia moyo katika kiu yao ya kusaka elimu.


Baadhi ya waombolezaji wamesema watamkumbuka kwa jitihada zake kuwapigania watu wa kata ya Kakunyu waliokuwa wakiporwa ardhi yao na watu wasiojali maisha ya watu wa kawaida, ujenzi wa daraja la Kabingo kwenye mto Ngono kuunganisha tarafa za Kiziba na Missenyi, na ujenzi wa madaraja kwenye tingatinga ( ardhi oevu) ya Kajai, kuruhusu kupitika mwaka mzima barabara ya Katoma- Kanyigo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso