Naibu Waziri wa Afya Dkt, Godwin Mollel amewataka wananchi kuepuka matumizi yasiyo sahihi ya vidonge vya kuzuia mimba maarufu kama P2 ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza pale dawa hizo zinapotumika bila utaratibu ikiwemo mvurugiko wa hedhi.
Dkt. Mollel amesema hayo leo Jijini Dodoma kwa niaba ya Waziri wa Afya Mhe, Ummy Mwalimu wakati akijibu swali Namba 163 ambapo swali hilo limeulizwa na Mbunge wa Viti Maalum Dkt, Thea Medard Ntara aliyeuliza Je, kuna mpango gani wa kuruhusu Sayana Press kama njia ya Uzazi wa Mpango badala ya kutumia P2 bila utaratibu.
“P2 ni njia ya dharura ya vidonge vya
uzazi wa mpango ambayo hutumika kuzuia mimba kwa mwanamke aliyefanya tendo la kujamiiana bila kinga kwa mfano aliyebakwa,
au aliyetumia kondomu ikapasuka na anadhani anaweza kupata
mimba asiyoitarajia wakati Sayana Press
ni njia ya kuzuia kupata ujauzito kwa muda mrefu,” aliseme
Dkt Mollel
Hata hivyo Dkt. Mollel ameongeza kuwa Sayana Press imesajiliwa na TMDA na inapatikana kwenye vituo binafsi vya kutolea huduma za afya kwa wateja wanaohitaji.
Chanzo : FullShangwe
No comments:
Post a Comment