AMCHINJA MKE WAKE MJAMZITO KISHA KUMTOBOA TUMBO NA KUTOA MAPACHA WAWILI UMRI WA MIMBA MIEZI 8 - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday 1 February 2024

AMCHINJA MKE WAKE MJAMZITO KISHA KUMTOBOA TUMBO NA KUTOA MAPACHA WAWILI UMRI WA MIMBA MIEZI 8

Jeshi la polisi mkoa wa Tabora linamshikilia Hamisi Kulwa (35) mkazi wa kata ya uyogo wilaya ya Urambo kwa tuhuma za kumchinja mke wake mjamzito na kumtoboa tumbo kisha  kuwatoa watoto mapacha na  kumpika mmoja wapo

Kamanda wa polisi mkoani Tabora  kamishna msaidizi Richard Abwao

Akizungumzia Tukio hilo  kamanda wa polisi mkoani Tabora  kamishna msaidizi Richard Abwao mbele ya waandishi wa habari amesema kuwa  tukio  hilo limelotokea januari 30 mwaka huu majira ya saa 11 jioni katika kitongoji cha Isunda kijiji cha milambo kata ya uyogo wilayani urambo mkoani Tabora


Amesema kuwa  mtuhumiwa   alifanya tukio  la  kumchinja mkewe na watoto watatu, watoto wawili mapacha waliokuwa  tumboni na mwingine mmoja aliyekuwa na umri wa miaka miwili kisha kuwazika na kiumbe kimoja alichokitoa tumboni  akakipika. 


 “Tulipomkamata  na  tulipoanza kumuhoji alisema kuwa aliambiwa kuna watu wanamuijia mke wake na watoto wanawapeleka Gamboshi kufanya kazi za kichawi kila siku usiku na siku sio nyingi watawaijia na kuwaua ndio maana akaamua awaue yeye mwenyewe” alisema Kamanda Abwao kwa ufafanuzi


Kamanda huyo amesema kuwa  jeshi la polisi  linaendelea na upelelezi mara baada ya kukamilika mtuhumiwa  atafikishwa  mahakamani kwa mujibu wa sheria


Hata hivyo kamanda  wa polisi mkoani Tabora ametoa wito  kwa wananchi wa kijiji hicho kuachana na imani potofu za kishirikina na kumwamini Mwenyezi Mungu   na kusisitiza kuwa   ndio njia pekee ya kuondokana na mauaji pia kuimarisha vikundi vya ulinzi shirikishi katani hapo.


Nae Diwani wa kata ya Uyogo, Ntoloki Kazimile amesema ameshangazwa na kitendo kama hicho  cha  bwana huyo kufanya unyama  kijijini hapo   na kuiomba serikali kuchukua hatua za haraka iwezekanavyo ili iwe fundisho kwa watu wengine.

Chanzo: Fullshangwe


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso