Bingwa mtetezi Senegal katika Kombe la Mataifa Afrika mwendo ameumaliza kwa kufungashiwa virago na Ivory Coast.
Senegal walikuwa ni mabingwa wa 2022 wa AFCON safari yao imegota mwisho baada ya kupoteza mbele ya Ivory Coast kwenye mchezo ambao walikuwa wakipewa nafasi kubwa ya kusonga hatua inayofuata.
Ilikuwa ni hatua ya 16wanaishia wakikwama kutinga robo fainali kwenye mchezo uliokuwa na ushindani mkubwa kwa kuchezwa dakika 12.
Ikumbukwe kwamba Januari 29 baada ya dakika 90 ngoma ilikuwa Senegal 1-1 Ivory Coast katika dakika 30 nyingine ngoma ilikuwa ngumu kwa timu zote.
Kwenye penalti Senegal yenye nyota Sadio Mane ilifunga 4-5 Ivory Coast ambao walitinga hatua ya 16 bora wanakwenda robo fainali na ni wenyeji wa mashindano hayo.
Mabao yalifungwa na Habib Diallo dakika ya 4 kwa Senegal na Franck Kessie dakika ya 86 kwa mkwaju kwa penalti.
No comments:
Post a Comment