RAIS WA ZAMANI JELA MIAKA MITANO - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday, 6 December 2023

RAIS WA ZAMANI JELA MIAKA MITANO

RAIS wa zamani wa Mauritania, Mohamed Ould Abdel Aziz amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela kwa kosa la utakatishaji fedha kipindi cha uongozi wake.



Abdel Aziz aliiongoza Mauritania kwa muongo mmoja baada ya kuingia madarakani katika mapinduzi ya 2008 na alikuwa mshirika wa madola ya Magharibi, alishtakiwa mwezi Januari na alikanusha madai ya ufisadi.


Mahakama ilimkuta na hatia Abdel Aziz ya mashtaka mawili kati ya 10, kufuatia uchunguzi wa madai ya ubadhirifu wa mali ya umma na ufisadi.


Mmoja wa mawakili wake aliita uamuzi huo “hukumu ya kisiasa inayomlenga mtu na familia yake”. Waendesha mashtaka walisema hukumu ya mkuu huyo wa zamani wa nchi ilikuwa ya kihistoria.


Mahakama hiyo iliwaachilia huru baadhi ya washirika wa Abdel Aziz ambao pia walishtakiwa wakiwemo mawaziri wakuu wawili wa zamani.

Chanzo: habarileo

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso