WAZIRI Mkuu wa zamani wa Rwanda na mkosoaji mkubwa wa serikali ya Rais Paul Kagame amefariki akiwa uhamishoni nchini Ubelgiji.
Ndugu walithibitisha kifo cha Faustin Twagiramungu, wakisema kiongozi huyo wa miaka 78 alikuwa mgonjwa.
Twagiramungu alikuwa waziri mkuu katika serikali ya umoja wa kitaifa ambayo iliundwa baada ya mauaji ya kimbari ya 1994.
Alitofautiana na serikali iliyotawaliwa na Watutsi alipozungumza dhidi ya mauaji ya Wahutu. Alijiuzulu wadhifa wake mnamo 1995 na kwenda uhamishoni Ubelgiji.
Chanzo: habarileo
No comments:
Post a Comment