DAR ES SALAAM: Tume ya Utumishi ya Walimu (TSC) imemsimamisha kazi aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Mwalimu Maganga Japhet, kwa utoro kazini na kukaidi maelekezo ya viongozi wake.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, Elihuruma Mabelya amesema katika taarifa leo Alhamis Disemba 7 kuwa, Maganga ambaye ni Mwalimu wa Shule ya Msingi Tandika amesimamishwa kazi kuanzia Disemba 5.
Maganga aliteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Mkoani Kagera lakini hakuitumikia nafasi hiyo. Hata hivyo alipoomba kibali cha kuendelea na nafasi yake ya Ukatibu Mkuu alikataliwa na mwajili wake alimtaka kurejea kwenye majukumu ya Ualimu mara moja kuanzia Oktoba 1, 2023
Alipaswa kurejea kwenye Cheo cha Mwalimu Mwandamizi Daraja A katika Manispaa ya Temeke baada ya maombi yake ya kuongeza muda wa kuazimwa kukataliwa. Aliomba kibali cha kuazimwa kuitumikia CWT (Agosti 21, 2017 hadi Septemba 30, 2020), akaomba tena Juni 1, 2020 na kumaliza muda wake Septemba 30, 2023, Mwalimu Maganga aliomba kibali kingine kwa mara ya tatu ndipo kikataliwa.
Chanzo: habarileo
No comments:
Post a Comment