WAZEE KATIKA KATA YA BUGANDIKA WILAYANI MISSENYI, WAFURAHIA KUONDOKANA NA HALI YA UPWEKE, WAJIVUNIA SACCOS YAO, WAJIANDAA NA HUDUMA ZA BIMA YA AFYA NA KUANZISHA DUKA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday, 15 September 2023

WAZEE KATIKA KATA YA BUGANDIKA WILAYANI MISSENYI, WAFURAHIA KUONDOKANA NA HALI YA UPWEKE, WAJIVUNIA SACCOS YAO, WAJIANDAA NA HUDUMA ZA BIMA YA AFYA NA KUANZISHA DUKA


Wazee wa kikundi cha BKKOLW'ENGONZI katika kata ya Bugandika wilayani Missenyi wanaofadhiliwa na SHINA Inc,Tanzania

Wazee wa kikundi cha BKKOLW'ENGONZI katika kata ya Bugandika wilayani Missenyi wanaofadhiliwa na SHINA Inc,Tanzania


Na Mutayoba Arbogast, HUHESO DIGITAL, Bukoba


Wazee 270 katika kata ya Bugandika, wilaya ya Missenyi, mkoani Kagera wanaosaidiwa na shirika lisilo la kiserikali la SHINA Inc, kuwaondoa katika hali ya upweke kwa kuwakutanisha pamoja kuwajengea uwezo wa kukabiliana na hali ya uzee, wameanzisha Chama chao cha kuweka na kukopa kilichosajiliwa kwa jina la Abalakimala Saccos.


Mwenyekiti wa kikundi hicho cha wazee hao wenye umri wa kuanzia miaka 70, kiitwacho 'BIKOLW'ENGONZI' Audax Rwegarulila, amesema kuwa kutokana na kiasi cha fedha kidogo kidogo ambacho wanajiwekea kwenye saccos yao wamelenga iwasaidie kuanzisha miradi mbalimbali ikiwemo kuanzisha duka la kikundi.


Aidha wazee hao wamesajili pia kikundi chao kama chama cha kijamii katika Halmashauri ya wilaya ya Missenyi.


Wazee hao wanafadhiliwa na Shirika la SHINA Inc, kuwaondoa katika hali ya upweke wa kutopea kwenye lindi la mawazo ambalo linaweza kuwaathiri kisaikolojia, na hivyo kuwaleta pamoja, ambapo hukutana mara mbili kwa mwezi kubadilishana mawazo, mazoezi ya mwili/viungo, kukumbushana mambo ya kale, kusimuliana hadithi na ngano, na michezo ya kujenga utimamu wa mwili na akili, ikiwemo kucheza bao na karata.


Rais wa SHINA Inc,lenye makao makuu yake makuu nchini Marekani likifanya kazi huko na Afrika pia, Jessica Kamala Mushala, amesema wazee hao wanajisikia faraja kwani kukutana kwao kunawaondolea msongo wa mawazo na kuondoa fikra hasi za kuona kwamba ukishakuwa mzee hakuna anayekujali.


Jessica ambaye ni mzaliwa wa kata hiyo ya Bugandika yupo hapa nchini kwa shughuli za kifamilia na kukutana,kuona na kuhimiza miradi ya maendeleo inayotekelezwa na shirika lake, ukiwemo mradi huo wa wazee.


"Nilimuona mama Ma Yuliana Kokwitika alivyotuhangaikia kutulea wanawe, kwa moyo wa upendo na uvumilivu, hata akaniambukiza moyo huo na mimi kupenda kutoa nilichonacho.Nilimuona pia wakati wa uzee wake akitembelewa na wanawake wenzaje kumfariji, nikajiuliza je ni kila mzee anaweza kupata fursa ya kutembelewa na kufarijiwa?!", anasema Bi Mushala ambaye amefuatana na mumewe ambaye pia ni Mlezi wa SHINA Inc, Amos Mushala.


Mkurugenzi wa SHINA Inc, Tanzani, Johanes Chamshala, amesema shirika linawagharamia usafiri wazee hao kwenda kituo cha kukutana na kurudi nyumbani, chai na chakula wawapo kituoni, na kuwa umoja wa wazee hao ulianza mwaka 2021, na kuwa ni kuanzia wazee wenye umri wa miaka 70, kwani hao wamechoka kuliko wale wa miaka 60.


Aidha amesema wazee hao wanayo akaunti ya benki kutokana na michango yao ya mwaka, ambapo mwisho wa mwaka, shirika huwaongezea fedha kiasi kilekile sawa na kilichomo kwenye akaunti yao.


Hitaji kubwa la wazee hao nikupata Bima ya Afya iliyoboreshwa kwa kuwa wengi wao hawana bima na hivyo kuwa nashakani pindi afya zao zinapotetereka, hivyo tayari shirika limekwishamleta mtaalam wa bima ambaye amewapa ufafanuzi na kuwa muda si mrefu wazee hao watajiunga na bima huku shirika likitafakari namna ya kusaidia.


Mlezi wa SHINA Inc Amos Mushala alipoulizwa iwapo shirika li tayari kuwajengea kituo cha kuwatunza wazee hao moja kwa moja, amesema wazee wataendelea kutunzwa na jamaa zao nyumbani, hawahitaji kuwatenga na familia, bali kuwasaidia tu kujumuka pamoja na kufurahia uzee wao kwa kuwapunguzia fikra nzito zinazoweza kuwaathiri.


Kwa Tanzanua SHINA Inc, linalo miradi kadhaa ikiwemo shule ya awali(na shule ya msingi inayoendelea kujengwa) ya ITIKA Preprimay and Primary school, iliyoko kata ya Bugorora wilayani Missenyi, inayotumia mchepuo wa Kiingereza, ambapo watoto wa darasa la awali hadi la tatu wanasomeshwa bure.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso