WAHUKUMIWA MIAKA SITA KWA KOSA LA KUIBA PIKIPIKI KWA KUVUNJA OFISI YA DMO - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday, 20 September 2023

WAHUKUMIWA MIAKA SITA KWA KOSA LA KUIBA PIKIPIKI KWA KUVUNJA OFISI YA DMO


Watu wawili akiwemo raia wa Burundi, Niyokindi Anthony (44), wamehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka sita jela baada ya kukiri kutenda kosa la kuvunja Ofisi ya Mganga Mkuu (DMO) Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza na kuiba pikipiki tatu zenye thamani ya Sh.Milioni 11,850,000.


Mshtakiwa mwingine aliyehukumiwa kutumikia kifungo hicho ni mkazi wa Isungangh’olo Wilaya ya Sengerema mkoani hapa Ibrahim Mshengezi (55) ambapo wamehukumiwa kwa kutenda makosa mawili ambayo ni kuvunja Ofisi na kuiba.


Katika kesi hiyo yenye washtakiwa watatu, mshtakiwa mwingine ambaye ni Mkazi wa Isungangh’olo Wilaya ya Sengerema, Anold Paul (25) amekana mashtaka hayo ambapo Hakimu Mkazi mwandamizi wa Mahakama hiyo, Evod Kisoka ameamuru arejeshwe rumande baada ya kukosa wadhamini.


Awali, akiwasomea maelezo ya kosa washtakiwa, mwendesha mashtaka wa Serikali, Sajenti wa Polisi Theophilius Bei amesema kuwa washtakiwa walitenda makosa hayo Agosti 20.2023, kwa kuiba pikipiki tatu za Serikali zenye namba za usajili, SM15342, SM15343 na SM15349, zote kampuni ya Yamaha kinyume na Kanuni ya adhabu Sura ya 16 toleo la Mwaka 2022.


Hata hivyo, shtaka dhidi ya mshtakiwa namba tatu (Anold Paul) ambaye amekana mashtaka hayo litaendelea Oktoba.2.2023

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso