KALIYANGO WA WILAYANI KAHAMA AHUKUMIWA MAISHA JELA KWA KOSA LA KUMNAJISI MTOTO - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday, 22 September 2023

KALIYANGO WA WILAYANI KAHAMA AHUKUMIWA MAISHA JELA KWA KOSA LA KUMNAJISI MTOTO


MAHAKAMA ya Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga imemuhukumu mkazi wa kijiji cha Chapulwa kata ya Mwendakulima Kaliyango Maganga (55) kifungo cha maisha jela kwa kukutwa na kosa la kumnajisi mtoto mwenye umri wa miaka minane anayesoma darasa la kwanza.


Hakimu mkazi wa mahakama hiyo, Christina Chovenye alitoa hukumu hiyo jana katika kesi jinai namba 240/2023 ambapo mshtakiwa alitenda kosa hilo mara kwa mara kwa mtoto huyo nakushtakiwa Julai 30, 2023.


Hakimu Chovenye alisema mshtakiwa alikuwa na kazi ya umwagiliaji bustani ya maua nyumba ya jirani ambapo alikuwa akimvizia wakati akienda shule.


“Walezi wake ambao ni babu na Bibi walikuwa wakiondoka nakumuacha ndipo mtuhumiwa alikuwa akimchukua na kumnajisi huku akimueleza asimwambie mtu akisema atamuua”alisema Chovenye.


Hakimu Chovenye alisema mtoto mwenyewe alisikilizwa na kutoa maelezo ya kunajisiwa na mtuhumiwa mara kwa mara na vipimo vya daktari vimethibitisha hivyo mahakama haikuwa na shaka lolote juu ya utoaji wa hukumu hiyo dhidi ya mshtakiwa.


Hakimu Chovenye alisema walimu wa shule anayosoma mtoto huyo walitoa maelezo ya kugundua mtoto huyo kunajisiwa nakueleza kila siku amekuwa akichelewa shule na akifika anakuwa amechoka na kuwa na maumivu makali.


Mwendesha mashtaka ambaye ni wakili wa serikali, Evodia Baimo alisema kesi hiyo imesikilizwa mara nne tangu kufunguliwa kwa shauri hilo na wamesikiliza na adhabu kwa mshtakiwa iko sahihi ili iwe fundisho kwa wengine.


Mshtakiwa Kaliyango Maganga akijitetea kwa upande wake aliomba kupunguziwa adhabu hiyo kwa madai ni mzee na anategemewa na familia.


CHANZO:HABARI LEO

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso