WATANZANIA WATAKIWA KUSHIRIKIANA NA OFISI YA WAZIRI MKUU - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday, 8 August 2023

WATANZANIA WATAKIWA KUSHIRIKIANA NA OFISI YA WAZIRI MKUU



NA PAUL KAYANDA-MBEYA


NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri mkuu,Sera, Bunge na Uratibu, Mhe. Ummy Nderinanga ameipongeza Ofisi ya Waziri mkuu, Sera,bunge na uratibu kwa kushiriki kwenye maonesho ya nane nane na kuleta idara zote zinazohusina na ofisi hiyo

Aidha Naibu Waziri huyo ametoa wito kwa watanzania wakiwemo wananchi wa Jiji la Mbeya na kwamba wajitokeze kupata maelezo dhidhi ya mapambano ya virusi vya Ukimwi na kuongeza kuwa lakini kwenye eneo la maafa Mkoa wa Mbeya maeneo ya Kyela na maeneo mengine huwa wanapata maafa hasa masuala ya mafuriko.


Mhe.Nderinanga ameyasema hayo baada ya kutembelea banda la Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu katika sherehe hizo za Nane Nane zinazofanyika Jijijini Mbeya.

Amesisitiza wananchi waendelee kufika banda la ofisi ya Waziri mkuu, Sera Bunge na Uratibu ili kujifunza zaidi wapate kujua namna ambavyo wanaweza kukabiliana kabla na baada na namna ambavyo serikali inaratibu kuanzia serikali kuu mkoa, wilaya na mpaka ngazi za chini kwenye eneo la maafa.


''Yote kwa yote programu ya kilimo na Uvuvi tupo katika hatua ya kufanya tathmini ya kipindi cha miaka mitanowaje wajifunze waone namna taratibu wizara zingine za kisekta za kilimo na uvuvi kuona namna nchi yetu inavyopiga hatua kwa mana hiyo mimi niwakaribishe Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, bunge na Uratibu tuendelee kushirikiana tuendelee kujifunza kazi zinazofanywa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu,'' amesema Mhe. Ummy Nderinanga .

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso