Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) limetoa wito kwa wananchi wote wanaomiliki au wanaouza mavazi, viatu, mabegi na vitu vinavyofanana na sare za majeshi nchini kuvisalimisha ndani ya siku saba kuanzia leo.
Wito huo umetangazwa leo Alhamisi Agosti 24, 2023 na Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano Makao Makuu ya jeshi hilo, Luteni Kanali Gaudentius Ilonda.
Luteni Kanali Ilonda amesema baada ya siku hizo saba kuisha atakayekutwa navyo atachukuliwa hatua za kisheria.
Amewataka wananchi, wasanii na wafanyabiashara wanaouza mavazi na vitu vingine vyenye rangi za sare za majeshi nchini, kusalimisha vitu hivyo katika makambi ya JWTZ, wenyeviti wa Serikali za Mitaa na vituo vya Jeshi la Polisi Nchini.
“Hatuna nia ya kumsumbua mwananchi, hatuna nia ya kuona mwananchi akipata kadhia lakini baada ya siku saba nyie wenyewe mtajionea vijana wetu watakuwa mtaani kwa kutumia busara, hekima na kufuata sheria kwa ajili ya kukusanya mavazi,”amesema
chanzo: Mwananchidigital tv
No comments:
Post a Comment