Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesema wachezaji 10 wa Azam pekee ndio majina yao yamewasilishwa vibali vyao na wanastahili kucheza michezo ya Ngao ya Jamii 2023 mkoani Tanga.
Katika taarifa hiyo iliyotolewa leo Agosti 9 imeeleza timu za Simba, Yanga na Singida Fountain Gate hazijawasilisja vibali vya wachezaji wa kigeni hiyo wachezaji hao hawataruhusiwa kucheza mashindano hayo yanayoanza leo kwa mechi ya Yanga vs Azam.
Wachezaji 10 wa kigeni wa Azam ambao majina yao yamewasilishwa ni Ali Ahamada, Daniel Amoah, Kipre Junior, Prince Dube, Malickou Ndoye, Idrissu Abdulai.
Wengine ni James Akaminko, Idris Mbombo, Allasane Diao na Cheick Sidebe.
No comments:
Post a Comment