Meneja Mauzo na Usambazaji kampuni ya mawasiliano TIGO Mkoa wa Mbeya, Ronald Richard amesema kuwa wanatumia fursa ya siku ya kilele cha maonesho ya kimataifa ya Nane nane 2023 katika Mkoa huo kuhamasisha wakulima kujiunga na TIGO ili kuwarahisishia shughuli za kilimo.
NA PAUL KAYANDA-MBEYA
Maonesho hayo yanafungwa rasmi leo Agost 8,2023 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan na kauri mbiu ya mwaka huu ikiwa "Vijana na wanawake ni msingi imara wa mifumo endelevu na chakula".
Aidha meneja mauzo na usambazaji katika kampuni hiyo, Richard amesema kuwa wanatumia vyema kilele cha maonesho hayo kuhamasisha wakulima kujiunga na huduma ya TIGO.
Amesema kuwa kwa sasa kampuni ya mawasiliano Tigo imeanza kulipa wakulima kwa mfumo wa TIGO PESA katika Wilaya ya Kyela ambako wanalima zao la kakao pia Wilaya ya Tunduru na Mtwara wanakolima zao la korosho.
Amewataka wananchi na wakulima hao kujiunga na huduma hiyo ili kurahisisha shughuli zao.
"Huduma hii inarahisisha shughuli za wakulima na ukilinganisha wengi wao wapo vijijini ambako hakuna huduma zakibenki lakini kwa kutumia tigo Pesa kulipa malipo yao inawapunguzia umbali mrefu kwenda kwenye huduma za kibenki,"alisema meneja mauzo na usambazaji Tigo.
Hata hivyo mmoja wa wakulima hao ambaye hakutaja jina lake amesema kuwa amefurahishwa na huduma ya Tigo hasa kupitia TIGO PESA ambapo wakulima wanalipwa pesa zao kupitia tigo pesa hiyo imerahisisha na kupunguza changamoto ya umbali na mabenki.
"Nimefurahishwa na huduma ya Tigo kupitia Tigo pesa na kupitia Wakulima kupata huduma ya kuingiziwa hela yao baada ya mauzo ya mazao yao kupitia Tigo Pesa wakulima wamefurahishwa sana na huduma hii," alisema mkulima huyo na kuongeza.
Amesema kuwa pia wakulima wamefurahishwa pia na huduma ya tigo kilimo wameipenda, kwamaana hiyo inarahisisha shughuli zao na kuomba huduma hiyo ienee kwa wakulima wote kupitia elimu hiyo inayotolewa na kampuni.
No comments:
Post a Comment