Jeshi la Niger linasema litamfungulia mashitaka Rais aliyeondolewa madarakani Mohamed Bazoum kwa uhaini, saa chache baada ya kundi la wanazuoni waandamizi wa Kiislamu kusema viongozi wa mapinduzi ya nchi hiyo wako tayari kwa diplomasia kutatua mzozo wao na jumuiya ya kikanda ya Afrika Magharibi. Katika taarifa yake iliyosomwa kwenye televisheni ya taifa jana Jumapili, msemaji wa jeshi la Niger alitaja mashtaka dhidi ya Bazoum kama "uhaini mkubwa na kudhoofisha usalama wa ndani na nje" wa nchi.
Bazoum, 63, na familia yake wamezuiliwa katika makazi rasmi ya rais huko Niamey tangu mapinduzi ya Julai 26, huku wasiwasi wa kimataifa ukiongezeka juu ya hali zao kizuizini.
Rais aliyeondolewa madarakani amesema kwamba matibabu ambayo yeye na familia yake wamepokea ni "ya kikatili'' lakini serikai ya kijeshi ilisema baada ya daktari kumtembelea Bazoum kwamba hakukuwa na matatizo yoyote kuhusu afya yake.
Kanali Maj Abdramane, ambaye alisoma taarifa hiyo, pia alishutumu "vikwazo haramu, vya kinyama na vya kufedhehesha vya Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (Ecowas)".
CHANZO:BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment