SERIKALI YAENDELEA KUTOA ELIMU YA SERIA YA USIMAMIZI WA MAAFA NAMBA SITA YA MWAKA 2022 - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday, 4 August 2023

SERIKALI YAENDELEA KUTOA ELIMU YA SERIA YA USIMAMIZI WA MAAFA NAMBA SITA YA MWAKA 2022


SERIKALI Kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Idara ya Menejimenti ya Maafa Inaendelea Kutoa Elimu kwa Umma Kuhusu Sheria ya Maafa No.6 ya Mwaka 2022 na Kanuni zake za Mwaka 2022 lakini pia Kuelezea Mkakati wa Taifa wa Usimamizi wa Maafa Pamoja na Miongozo na Mipango Inayoelezea Shughuli za Usimamizi wa Maafa Nchini.


NA PAUL KAYANDA


Kitengo Cha Idara ya Menejimenti ya Maafa ni Mojawapo ya Idara katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu inayoshiriki katika Sherehe za maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nane Nane 2023 ambayo yanafanyika katika viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya.


Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa, Charles Msangi alisema hayo Agost 3,2023 mbele ya Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa alipotembelea Banda la Ofisi ya Waziri Mkuu ambapo alisema kuwa Kwa Upande wa Ofisi ya Waziri Mkuu wamekuja kwaajili ya kutoa Elimu kwa Umma Hasa kuhusu Sheria ya Usimamizi wa Maafa Na.6 ya Mwaka 2022 Na kanuni zake za Mwaka 2022 Lakini pia kuelezea Kuhusu Mkakati wa Taifa wa Usimamizi wa Maafa Pamoja na Miongozo na Mipango zinazoelezea Usimamizi wa Maafa kwa Kushirikisha wadau.


Msangi alisema kuwa wanatoa Elimu hii ili kuhakikisha kuwa Taasisi zote Zikiwemo Idara na Taasisi za Serikali Lakini Pia Wadau wa Sekta Binafsi Wanajua Majukumu yao kwa Mujibu wa Sheria Na.6 ya Mwaka 2022 lakini Ushiriki wao katika Muundo wa Uratibu na Usimamizi wa Maafa Ambao Kuanzia Ngazi ya Taifa kuna Kamati za Taifa za Usimamizi wa Maafa Lakini wana Kamati hizi ngazi ya Mkoa, Wilaya mpaka Ngazi ya Vijiji kutokana na Hali hiyo Lengo Kubwa ni Kutoa Elimu kuhusu huo mfumo na Muundo huo unaoshughulika na shughuli za Maafa ambazo zimejikita katika hatua zote kuanzia Hatua za awali za kuzuia na Kupunguza Madhara ya Majanga.


''Tunaelewa kabisa majanga yapo aina mbili, kuna yale Majanga yanayosababishwa na shughuli za asili kama Matetemeko, Mafuriko ambayo kimsingi Majanga haya hatuwezi kuyazuia lakini katika Shughuli zetu tunazozifanya za maendeleo basi kuna hatua zinaweza zikafanyika kwaajili ya kupunguza Madhara ama athari zake, Lakini kuna haya madhara mengine yanayosababishwa na Shughuli za kibinadamu haya kwa kiasi kikubwa Tunaweza Kuyazuia kabisa yasiutokee na kuleta Madhara kwa Binadamu kwa hiyo, Ushiriki wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu ni kwaajili ya kutoa Elimu kuhusu Majanga hayo na namna Hatua za Kuchukua kwa Mujibu wa Sera, Sheria na Taratibu, Lakini pia Tumeweka Mpango wa kutoa Elimu kwa Mwananchi mmoja mmoja kwa sababu tunaelewa suala la Usimamizi wa Maafa linaanza na mtu binafsi,'' alisema Msangi.


Aidha Mkurugenzi huyo Msaidizi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa, Msangi alisema kuwa suala la Mafuriko limekuwa likitokea katika miji mingi lakini lakini sababu zake zinaweza kuzuilika au zinazweza zikapunguza madhara,Na kuhakikisha kuwa Wananchi wanakaa katika maeneo salama lakini pia kuhakikisha kuwa mazingira yanakuwa Safi ili maji yasije kuleta Madhara, Lakini Kuna majanga Mengine Kama Ukame,Tetemeko la Ardhi na kwamba hayo ndiyo maelezo ya kawaida kabisa yanayotolewa na Hatua ambazo ni za kawaida kabisa za Mfumo wa Maisha ya kila siku kwa binadamu.


Pia Alifafanua kuwa katika sherehe za Maadhimisho hayo ya Nane Nane kwa Elimu ya Mtu Mmojammoja wapo wataalamu katika banda hilo kwaajili ya kueleza lakini pia vimeandaliwa vipeperushi ambavyo vinaeleza Rugha nyepesi kuhusu hayo Majanga ambayo yanaeleza Wajibu kwa mtu Mmoja Mmoja lakini nayeye pia anaweza akashirikiana vipi katika kuhakikisha kwamba kwa Serikali za Mitaa katika Ngazi za Vitongoji Wanaweza kuchukua hatua gani kwa kushirikiana Wao kama wao kama Wananchi na kwamba vipeperushi vipo wanagawiwa na wataalamu waliopo wanakuwa wanatoa maelezo namna gani bora ya kupunguza Madhara ama kuzuia Majanga yasilete Madhara kwa Binadamu Lakini na Ushiriki wao pia Pindi Matukio yanapotokea kwa kuwa wao ndiyo walengwa kwa mana hiyo wao ndiyo wanawajibu katika kusaidia pale majanga yanapotokea kwenye maeneo yao.


''Tunashukuru Kwa Kweli maandalizi ya maonesho yamekuwa Mazuri Wananchi Wamekuwa na mwitikio mkubwa na Tangu tumekuwepo hapa wananchi wamekuwa wakifika kwenye banda letu na kupewa Elimu,'' alisema Msangi.


Hata hivyo Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa akizindua Benki ya BOT aliwataka Wakuu wa Miko, pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri kutenga maeneo kwaajili ya shamba darasa ili vijana wajifunze masuala ya kilimo hatua ambayo itasaidia kuchangia vijana wengi kupata elimu hiyo na baadaye kukuza ajira nyingi kupitia sekta ya kilimo nchini.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso