Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Agosti 18, 2023 ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya Kigamboni kuchunguza mgogoro wa Ardhi Mtaa wa Muhimbili na Kichangani- Wilaya hiyo.
RC Chalamila amekitaka chombo hicho kuanza kuchunguza uhalali wa kiasi cha milioni 800 iliyolipwa na makazi kwa Ndg Julius Maganga, pili kuchunguza kodi ya Serikali kama ililipwa na wapi, vilevile kutumia hadidu za rejea za ripoti ya awali ambazo ziko tayari kuanza kuchunguza taarifa hizo ” TAKUKURU tumieni mamlaka zenu zote” Alisema Mhe Chalamila
Aidha RC Chalamila ameagiza Ofisi ya Naibu Kamishna wa Ardhi Mkoa huo kusitisha mara moja utoaji wa Hati za Ardhi katika eneo hilo kuanzia leo Agosti 18, 2023, Hata hivyo amemtaka Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni kuanza kufanya uhakiki wa wamiliki wote wa Ardhi katika maeneo mbalimbali ya Wilaya hiyo ili kukabiliana na utapeli wa Ardhi katika Wilaya hiyo.
Sambamba na hilo RC Chalamila amewataka Wakuu wa Wilaya zote 5 katika Mkoa huo kuanzisha Kliniki za Ardhi katika maeneo yao ili kutatua migogoro mbalimbali ya Ardhi kama anavyofanya Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe Halima Bulembo
Vilevile Naibu Kamishna wa Ardhi Mkoa wa Dar es Salaam Bwana Shukrani Kyando akitoa ufafanuzi wa kitaalam amesema kutokana na taarifa zilizoko ni wazi taratibu Stahiki hazikufuatwa za umiliki wa eneo hilo, viko viashiria vya kufoji nyaraka na udanganyifu hivyo Ofisi yake iko tayari kutoa ushirikiano kwa vyombo na kupokea maelekezo ya Mhe Mkuu wa Mkoa.
Mwisho Dhamira ya Serikali ni kumaliza migogoro ya Ardhi hivyo RC Chalamila ameelekeza yeyote atakayekataa kutoa ushirikiano apatiwe taarifa mara moja.
No comments:
Post a Comment